• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyakazi wanne wa msaada wauawa nchini Somalia katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-07-06 18:31:14

    Mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wanaotoa msaada wa bidhaa nchini Somalia yamesababisha vifo vya wafanyakazi wanne kati ya Januari na June mwaka huu.

    Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu OCHA imesema, zaidi ya matukio 90 ya kimabavu yaliwakuta maofisa wanaotoa misaada ya kibinadamu, vituo, na mali na kusababisha majeruhi kwa watu wanane, kukamatwa na kuzuiliwa kwa muda kwa wafanyakazi sita, na wengine 13 kutekwa nyara.

    Ofisi hiyo imesema, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, wafanyakazi 7 wa misaada ya kibinadamu wamefukuzwa na mamlaka nchini Somalia, na pia kumekuwa na ongezeko la matukio ya kutumia silaha yanayohusiana na mgao wa misaada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako