• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China akutana na rais wa Korea Kusini nchini Ujerumani

    (GMT+08:00) 2017-07-06 18:38:09

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na rais Moon Jae-in wa Korea Kusini mjini Berlin, Ujerumani.

    Katika mazungumzo yao, rais Xi amesema China inatilia mkazo uhusiano na Korea Kusini, na inashikilia msimamo wa kuendeleza urafiki na nchi hiyo. Pia amesema China inapenda kuuhimiza uhusiano huo kurudi kwenye njia nzuri yenye maendeleo ya utulivu kwa kutumia fursa ya miaka 25 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi.

    Kwa upande wake, rais Moon Jae-in amesema nchi yake inapenda kuimarisha mawasiliano ya ngazi ya juu na ushirikiano wa pande mbalimbali na China, na kujenga uhusiano wa wenzi wa kimkakati na China.

    Wakati huohuo, mwenyekiti wa Chama cha jamii na demokrasia cha Ujerumani Bw. Martin Schulz amekutana na rais Xi Jinping wa China, na kusema Ujerumani inatilia maanani umuhimu wa China kwenye masuala ya kimataifa. Naye rais Xi amesifu mchango uliotolewa na Chama cha jamii na demokrasia cha Ujerumani kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako