• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Alex Sanchez ataja dau lake ili asajiliwe na Arsenal

  (GMT+08:00) 2017-07-07 09:39:09

  Siku moja baada ya club ya Arsenal kutangaza kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa aliyekuwa anaichezea Olympique Lyon ya Ufaransa Alexandre Lacazette, jana mshambuliaji wa Arsenal raia wa Chile Alex Sanchez ameripotiwa kutaja mapendekezo yake ili asaini mkataba mpya.

  Sanchez ambaye alijiunga na Arsenal mwaka 2014 akitokea FC Barcelona ya Hispania, ametajwa kudai alipwe mshahara wa pound laki 4 kwa wiki ili asaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Arsenal.

  Inaripotiwa kuwa Arsenal wapo tayari kumlipa Sanchez zaidi ya pound laki 2.75 ambazo inaripotiwa ameahidiwa na Man City wakati FC Bayern Munich ambao wanamuhitaji wanasitasita kutoa ofa ya kiasi hicho cha mshahara licha ya kuonesha dhamira ya wazi ya kuhitaji huduma yake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako