• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Fainali ya Michuano ya COSAFA ni Zambia dhidi ya Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2017-07-07 09:40:39

    Michuano ya COSAFA Castle Cup inayoendelea huko nchini Afrika Kusini inaelekea kufikia ukingoni baada ya hapo juzi kushuhudia baadhi ya timu zikitinga hatua ya Fainali ya michuano hiyo.

    Timu ya taifa ya Zambia (Chipolopolo) imekuwa ya kwanza kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga Taifa Stars kwa jumla ya magoli 4-2 katika hatua ya Nusu Fainali mchezo ulichezwa katika dimba la Moruleng nchini Afrika Kusini.

    Wakati Zimbabwe imetinga hatua ya Fainali baada ya kuifunga timu ya taifa ya Lesotho kwa jumla ya magoli 4-3 kwa matokeo hayo inaifanya Zimbabwe kucheza na Zambia katika mchezo wa fainali utakao chezwa siku ya Jumapili Julai 9.

    Mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo ya COSAFA Castle Cup utazikutanisha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Lesotho leo Ijumaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako