• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usajili wa Romelu Lukaku Man United wamwacha Alvaro Morata njia panda

    (GMT+08:00) 2017-07-07 09:41:05

    Uamuzi wa ghafla wa Manchester United kumnunua Romelu Lukaku umemuwacha Alvaro Morata katika njia panda.

    Mshambuliaji huyo wa Real Madrid hadi juzi Jumatano alikuwa anajua kwamba amebakisha siku tu ili kuwa mchezaji wa Man United na kwamba wiki ijayo atajiunga na kikosi hicho kwenda ziarani Marekani Lakini baada ya United kukamilisha dili la £75m kwa Lukaku, Morata ameachwa mataani na kuendelea kubaki Real Madrild.

    Hivi sasa Morata anategemea kwamba Chelsea itarejea na kumchukua na kutumia pesa walizokusudia kuzitumia kwa Lukaku, kabla ya kuzidiwa nguvu na United wiki hii. Kama Morata ataishia Stamford Bridge itaonesha mapenzi ya miaka mingi aliyonayo kocha Antonio Conte kwa Morata.

    Antonio Conte anamtaka Morata kwa muda mrefu na kutarajia kumsaini baada ya kuanza kuitumikia Chelsea mwaka 2016. Hata Morata naye, pia anapenda sana kucheza chini ya kocha Conte tangu alipokuwa Juventus.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako