• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonyesho ya biashara ya Kenya kusheheni bidhaa zilizozalishwa ndani

    (GMT+08:00) 2017-07-07 09:51:50

    Maonyesho ya biashara ya Kenya yanayotarajiwa kufanyika kwa siku tatu yanatarajiwa kusheheni bidhaa zilizozalishwa ndani ya nchi.

    Katibu mkuu wa idara ya biashara ya taifa Bw Chris Kiptoo amewaambia waandishi wa habari kuwa maonyesho hayo yana lengo la kuimarisha hadhi ya Kenya kama kituo cha biashara na uzalishaji kwenye nchi za Afrika mashariki.

    Bw Kiptoo amesema mbali na maonyesho hayo, pia kutakuwa na mabaraza yatakayojadili kuhimiza biashara kupitia usafirishaji na ugavi, na kuhimiza nguvu ya Kenya ya uuzaji nje bidhaa zake, wakati kukiwa na ushindani kutoka nchi jirani.

    Maonyesho hayo yatafanyika wakati maonyesho ya biashara ya China na Kenya yanavutia mamia ya makampuni ya China kuonyesha bidhaa zao, zikiwa ni pamoja na bidhaa za walaji, vifaa vya ujenzi na vifaa vya umeme.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako