• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika matatu ya kimataifa yatoa wito kwa kundi la G20 kusukuma mbele utandawazi wa biashara

    (GMT+08:00) 2017-07-07 16:27:25

    Wakurugenzi wa Shirika la Mfuko wa Fedha la Kimataifa (IMF), Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Biashara Duniani (WTO) wametoa wito kwa viongozi wa nchi za kundi la G20 kuchukua hatua kusukuma mbele utandawazi wa biashara ili kuhimiza ongezeko la uchumi wa dunia.

    Taarifa ya pamoja iliyotolewa na wakurugenzi hao imesema, nchi mbalimbali zinapaswa kuondoa vizuizi vya kibiashara na kupunguza hatua za kujilinda zinazoharibu maendeleo ya biashara. Pia wametoa wito wa kutoa mafunzo ya ajira na ufundi kwa wafanyakazi walioathiriwa na maendeleo ya biashara na ufundi na kuboresha miundombinu ili kuongeza uhamishaji wa nguvukazi.

    Habari zinasema, tangu mwanzoni mwa mwaka 2000, makundi ya mbalimbali ya kiuchumi yalisimamisha ufunguzi wa kibiashara na kuendelea kutekeleza sera ya kulinda makampuni ya kienyeji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako