• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Singapore na meya wa mji wa Hamburg

    (GMT+08:00) 2017-07-07 18:38:33

    Rais Xi Jinping wa China amepokutana na waziri mkuu wa Singapore Bw. Lee Hsien Loong mjini Hamburg, Ujerumani.

    Katika mazungumzo yao, rais Xi amesema Singapore ni mratibu wa uhusiano kati ya China na Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki ASEAN, na mwakani itakuwa nchi mwenyekiti wa zamu wa jumuiya hiyo. Amesema China inaunga mkono kazi zinazofanywa na Singapore, na inaamini kwamba Singapore itasukuma mbele ushirikiano wa kihalisi kati ya China na ASEAN na mchakato wa utandawazi wa kikanda.

    Rais Xi Jinping pia amekutana na meya wa mji wa Hamburg Bw. Olaf Scholz. Amesema China inakaribisha mji huo kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na kuongeza uhai kwa uhusiano kati ya pande mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako