• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanafunzi wa kundi la kwanza wenye shahada ya uzamili wahitimu kutoka chuo cha ushirikiano na maendeleo kati ya kusini na kusini

    (GMT+08:00) 2017-07-07 19:06:25

    Wizara ya biashara ya China na Chuo kikuu cha Beijing jana kwa pamoja walifanya sherehe ya kuhitimu kwa wahitimu wa kundi la kwanza wa shahada ya uzamili wa chuo cha ushirikiano na maendeleo kati ya kusini na kusini, ikiwa ni pamoja na wanafunzi wenye shahada ya uzamili kutoka nchi 16 zinazoendelea zikiwemo Cambodia, East Timor na Ethiopia.

    Kwenye mikutano mfululizo inayoadhimisha miaka 70 tangu Umoja wa Mataifa ulipoanzishwa, Rais Xi Jinping wa China alitangaza hatua nyingi ikiwemo kuanzisha chuo cha ushirikiano na maendeleo kati ya kusini na kusini, na kuweka mpango wa kuimarisha ushirikiano wa kusini na kusini na kupata maendeleo ya pamoja.

    Chuo cha ushirikiano na maendeleo ya kusini na kusini kilianzishwa rasmi mwezi Aprili mwaka 2016, ambapo kiliandikishwa na wanafunzi 48.

    Kwenye sherehe hiyo, naibu waziri wa biashara wa China Bw. Yu Jianhua amewataka wahitimu waendelee kufuatilia shughuli za ushirikiano kati ya kusini na kusini baada ya kurudi katika nchi zao, kufuatilia ujenzi wa chuo cha ushirikiano na maendeleo kati ya kusini na kusini, na kuwashawishi wanafunzi wengi zaidi kusoma nchini China.

    Mhitimu kutoka Cambodia Bw. Vichda Long amesema, ananufaika sana na muda wa mwaka mmoja ambapo anasoma katika chuo cha ushirikiano na maendeleo kati ya kusini na kusini, atatumia alivyojifunza katika kazi yake katika siku za baadaye. Anasema,

    "Nimejifunza uzoefu wa maendeleo ya China. Maendeleo ya China ni ajabu. Kwa kupitia utungaji wa sera sahihi na jitihada za serikali na wananchi wake, China imekuwa moja ya makundi makubwa ya uchumi duniani ndani ya miaka 30 tu. Masomo hapa ni pamoja na vitu vyote muhimu husika na maendeleo ya taifa. "

    Bw Awan Riak kutoka Sudan Kusini amesema, kupitia masomo katika chuo hicho nchini China, ametambua kuwa ni muhimu sana kwa nchi moja kutafuta njia ya maendeleo inayoambatana na hali halisi yake. Anasema,

    "Nilipata mafanikio makubwa katika kujifunza uzoefu wa kukuza uchumi nchini China, uzoefu wa maendeleo ya miji na utamaduni wa China. Naona huu ni mradi muhimu unaoweza kunisaidia kihalisi."

    Chuo cha ushirikiano na maendeleo kati kusini na kusini kilizinduliwa mwezi Aprili mwaka 2016 kwenye taasisi ya maendeleo ya taifa ya Chuo Kikuu cha Beijing, ili kujenga kituo cha msingi cha kuandaa watu wenye ujuzi wa ngazi ya juu kwa nchi zinazoendelea, na kuweka mazingira kwa nchi zinazoendelea kufanya mawasiliano, na kutoa msaada wa watu wenye ujuzi kuhimiza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, kuhimiza nchi zinazoendelea zitimize mafungamano ya kisasa ya mfumo na uwezo wa usimamizi wa utawala wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako