• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lalaani mashambulizi ya kigaidi huko Rafah, Misri

    (GMT+08:00) 2017-07-08 17:10:24

    Baraza la usalama la umoja wa mataifa ijumaa limelaani shambulizi la kigaidi lililotokea katika mji wa Rafah Egypt ambapo karibu askari 10 wa Misri wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

    Wajumbe wa baraza hilo wamewahimiza wanachama wote wa ushirikiano wa kimataifa kushirikiana kikamilifu na Misri na mamlaka nyingine husika kufuatilia wahalifu, waandaaji, wafadhili na wadhamini wa vitendo vya kigaidi na kuthibitisha kuwa ugaidi ni tishio kubwa kwa amani na usalama wa kimataifa.

    Mapema, chanzo cha usalama cha Misri kililiambia shirika la habari la China Xinhua, kuwa askari hao waliuawa na wengine ishirini kujeruhiwa katika milipuko miwili ya gari na mashambulizi yaliyotokea baadaye kwenye kituo cha kijeshi cha ukaguzi mjini Rafah, kaskazini mwa Sinai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako