• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping kwa nyakati tofauti akutana na viongozi wa Uingereza, Japan na Ufaransang wa China

    (GMT+08:00) 2017-07-08 19:46:48

    Rais Xi Jinping wa China huko Hamburg, Ujerumani kwa nyakati tofauti amekutana na viongozi wa Uingereza, Japan na Ufaransa.

    Wakati rais Xi alipokutana na waziri mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May amesema chini ya juhudi za pamoja za China na Uingereza, pande hizo mbili zitaimarisha kuaminiana kimkakati, na ushirikiano wenye ufanisi katika sekta mbalimbali utapanda katika ngazi ya juu zaidi. China inapenda kushirikiana na Uingereza, kuhimiza uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote, na kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili.

    Bi. Theresa May amesisitiza kuwa Uingereza inapenda kutumia vya kutosha utaratibu wa mazungumzo kati ya viongozi wa nchi hizo mbili, na kuimarisha ushirikiano Pia Uingereza inapenda kushiriki katika ushirikiano wa fedha chini ya mfumo wa pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja".

    Wakati wa mazungumzo na waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe, rais Xi amesisitiza kuwa kulinda vizuri msingi wa siasa ni msingi wa kuendeleza uhusiano kati ya China na Japan. China inatumai Japan kufuata kanuni zilizowekwa kati ya pande hizo mbili kuhusu mambo ya historia ya suala la Taiwan.

    Katika mazungumzo na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, rais Xi amesema China inapenda kuendeleza ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta za uendelezaji wa nishati ya nyuklia na usafiri wa ndege, kupanua ushirikiano katika sketa za kilimo, chakula, fedha na maendeleo endelevu.

    Naye Rais Macron ameeleza kuwa Ufaransa inapenda kuimarisha ushirikiano n na kutakuza ushirikiano chini ya mfumo wa Umoja wa Mataifa ili kuhimiza amani na ustawi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako