• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pakistan na India zapambana kwenye eneo la Kashmir

    (GMT+08:00) 2017-07-09 18:30:20

    Majeshi ya Pakistan na India yamepambana kwenye eneo la Kashmir, pande hizo mbili kila mmoja akilaani upande mwingine na kusababisha vifo na majeruhi.

    Idara ya habari ya jeshi la Pakistan ilitoa taarifa ikisema kuwa jeshi la India lilitumia silaha nyepesi na nzito na mizinga kuushambulia upande wa Pakistan kwenye mpaka wa kudhibiti bila ya sababu, na kusababisha vifo vya wa raia wawili wa Pakistan na wengine watatu kujeruhiwa. Baadaye jeshi la Pakistan lilijibu shambulizi la India.

    Wizara ya mambo ya nje ya Pakistan imemwita naibu mjumbe mwandamizi wa India nchini Pakistan na kulaani kuwa jeshi la India lilikwenda kinyume na kanuni ya binadamu ya kimataifa kwa kuwashambulia raia wasio na hatia, linapaswa kulaumiwa.

    Msemaji wa wizara ya ulinzi ya taifa ya India Bw. Manish Mehta alisema kuwa jeshi la Pakistan siku hiyo alafajiri lilishambulia eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India, baadaye jeshi la India lilijibu shambulizi la Pakistan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako