• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yataka juhudi zaidi za G20 juu ya maendeleo ya Afrika, na uchumi wa kidigitali

    (GMT+08:00) 2017-07-09 19:24:17

    Rais Xi Jinping wa China amerudi Beijing leo baada ya kufanya ziara katika nchi za Russia na Ujerumani na kushiriki katika Mkutano wa 12 wa viongozi wa kundi la G20.

    Wakati wa mkutano huo, rais Xi Jinping aliwahimiza viongozi wa nchi tajiri na zile zinazostawi kiuchumi za kundi la G20 kuendeleza jitihada za kusaidia maendeleo ya Afrika na kujenga uchumi wa kidigitali kwenye mkutano wa siku mbili unaofanyika mjini Hamburg Ujerumani.

    Xi amesema kuunga mkono maendeleo ya Afrika ni muhimu kwa kukuza ukuaji wa uchumi unaozingatia uwiano na umoja, na kuwataka wanachama wa G20 kushiriki kikamilifu mpango waliokubaliana mwaka jana, kwenye mkutano wa kilele huko Hangzhou, China kwa kuunga mkono viwanda vya Afrika na nchi za maendeleo ya chini.

    Rais Xi ameeleza kuwa, China ni mpenzi wa dhati wa Afrika na hufuata kanuni za uaminifu, matokeo ya vitendo, ushirika na imani nzuri katika kushughulika na mahusiano na Afrika. Akiongeza kuwa China inasaidia maendeleo ya Afrika kwa njia ya miradi halisi ambayo hakuna masharti ya kisiasa yaliyowekwa.

    Xi amesisitiza kuwa wanachama wa G20 wanapaswa kujenga uchumi wa kidigitali ambao ni kirafiki kwa ukuaji na ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako