• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji waliosalia huko Benghazi bado wanaendelea na mapambano

    (GMT+08:00) 2017-07-10 09:28:24

    Msemaji wa jeshi la Libya kanali Miloud Zwei amesema wapiganaji waliosalia mjini Benghazi bado wanaendelea na mapambano, siku kadhaa baada ya kamanda wa jeshi hilo jenerali Khalifa Haftar kutangaza kukombolewa kwa mji huo. Bw. Zwei amesema mapambano bado yanaendelea katikati ya mji wa Benghazi, walikosalia wapiganaji wa mwisho. Jumatano iliyopita kamanda wa jeshi meja jenerali Khalifa Haftar alitangaza udhibiti kamili wa mji wa Benghazi na kuyashinda makundi ya wapiganaji baada ya mapambano ya miaka mitatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako