• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya aahidi kuimarisha usalama kwenye mkoa uliovamiwa na majambazi

    (GMT+08:00) 2017-07-10 09:44:21

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameahidi kuimarisha usalama kwenye kaunti ya Baringo iliyovamiwa na majambazi na katika siku za karibuni kukumbwa na matukio ya vurugu.

    Akihutubia mkutano wa kampeni huko Kabartonjo na Marigat, Rais Kenyatta amesema serikali yake itaimarisha usalama katika nchi nzima, na kusisitiza kuwa hawatalegalega kwenye masuala ya usalama baada ya waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery kufariki Jumamosi. Kenyatta pia ameeleza kuwa serikali yake itachukua hatua ya kuwalinda Wakenya, na kwamba hawatatoa nafasi kwa majambazi kuendeleza mauaji.

    Hivi sasa serikali imeimarisha usalama kwenye kaunti za Baringo na Turkana baada ya majambazi wenye silaha kuwauwa wanakijiji na kuiba mifugo yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako