• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Trump akutana na Rais Putin kando ya mkutano wa G20

    (GMT+08:00) 2017-07-10 09:57:45

    Rais Donald Trump amekutana na mwenzake wa Russia Vladimir Putin kando ya mkutano wa wakuu wa kundi la G20 uliofanyika Hamburg, Ujerumani.

    Baada ya mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw Sergey Lavrov amesema rais Trump amekubali kauli ya Rais Putin kuhusu Russia kutoingilia uchaguzi mkuu wa Marekani. Rais Putin amesema amejibu maswali ya Rais Donald Trump ambaye ameridhishwa na majibu yake.

    Rais Trump amesema amejadiliana na Rais Putin na kupanga kuweka mfumo wa kulinda usalama wa mtandao wa internet ili kuzuia mambo yanayoharibu usalama wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako