• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Somalia ataja mafanikio ya serikali yake wakati akifungua mkutano wa bunge

    (GMT+08:00) 2017-07-10 09:58:50

    Rais Mohamed Abdullahi Farmajo wa Somalia amefungua mkutano wa pili wa bunge baada ya bunge kuahirishwa kwa miezi miwili, huku akitaja mafanikio ya serikali yake tangu aingie madarakani.

    Akihutubia mabaraza yote ya bunge Rais Farmajo amesema serikali yake imeweza kuwalipa mishahara wafanyakazi wake kwa wakati na kujitahidi kuzuia uingizaji haramu wa silaha nchini Somalia. Pia amesema serikali yake imefanikiwa kujenga kikosi cha ulinzi wa mji wa Mogadishu na kuimarisha serikali kuu na serikali za majimbo.

    Wakati huo huo mjumbe mwandamizi wa umoja wa mataifa nchini Somalia Bw Michael Keating amekaribisha kufunguliwa kwa mkutano wa bunge na kuwataka wabunge watimize matumaini ya watu wa Somalia. Amesema bunge linaweza kutoa mchango kwenye kupitisha sheria ya uchaguzi na sheria za kuisaidia serikali kuongeza mapatao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako