• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya yatekeleza amri ya kutotembea usiku kwenye kaunti zilizoathiriwa na ugaidi

    (GMT+08:00) 2017-07-10 09:59:09

    Serikali ya Kenya imetangaza amri ya kutotembea usiku kwa muda wa miezi mitatu kufuatia kuongezeka kwa mashambulizi ya kigaidi kwenye kaunti zilizoko kwenye mpaka na Somalia.

    Kaimu waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Bw Fred Matiang'i amesema amri ya kutotoka nje kuanzia saa 12 na nusu jioni hadi saa 12 na nusu asubuhi, itatekelezwa hadi tarehe 9 Oktoba kwenye kaunti za Lamu na Garissa.

    Watu kumi waliuawa kwa kuchinjwa na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab kwenye mji wa Pandaguo katika kaunti ya Lamu, wiki moja baada ya wapiganaji wa kundi hilo kuvamia kituo cha polisi na kuwaua polisi watatu na kuwajeruhi wengine.

    Bw Matiang'i amesema amri hiyo haitahusu hoteli za kitalii kwenye maeneo ya Pate, Lamu na Manda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako