• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yataka kuanzisha tume huru ya haki za binadamu

    (GMT+08:00) 2017-07-10 10:03:08

    Somalia imezindua awamu ya kwanza ya mchakato wa taifa wa haki za binadamu, hatua inayoonekana kama kuwa ni mwelekeo wa kuimarisha ulinzi na haki za binadamu nchini humo.

    Waziri wa wanawake na maendeleo ya haki za binadamu Deqa Yasin amesema licha ya changamoto za usalama, umaskini au ukame, kuongeza mfumo wa haki za binadamu ni moja ya vipaumbele kwa serikali ya Somalia.

    Wizara hiyo imehusisha serikali za majimbo, mashirika ya kiraia na wadau husika kuanzisha jopo la uteuzi wa kiufundi (TSP) kwa mujibu wa sheria ya tume ya haki za binadamu (HRC Law).

    Katika awamu ya pili na ya mwisho, jopo hilo litatekeleza mchakato huo kwa njia ya usajili na kukaguliwa kwa walioopendekezwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako