• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yashindwa kuadhimisha sherehe za Uhuru kutokana na mgogoro unaoendelea

    (GMT+08:00) 2017-07-10 10:03:26

    Sudan Kusini imeonyesha masikitiko kutokana na kushindwa kwa mwaka wa pili mfululizo kuadhimisha sherehe za uhuru Julai 9, ambapo nchi hiyo inaadhimisha miaka 6 tangu ipate uhuru.

    Serikali ya Rais salva kiir imeeleza haikuweza kusherehekea uhuru wa mwaka huu katika mji mkuu wa Juba kutokana na matatizo ya kiuchumi baada ya mgogoro uliosababisha uzalishaji wa mafuta, ambao ni chanzo kikuu cha mapato, kupungua.

    Kamishna mmoja kutoka jimbo la kaskazini la Jonglei Bwana Dau Akoi Jurkuch amesema vurugu zinazoendelea zilisababishwa na tofauti za kisiasa kati ya Rais Kiir na makamu wake wa kwanza wa zamani katika serikali ya mpito, na kutoa wito umoja na mazungumzo.

    Umoja wa Mataifa umeonya kuwa ingawa Sudan Kusini ilitajwa kumaliza baa la njaa, zaidi ya watu milioni 7 wanakabiliwa na hali ya ukame na njaa kama misaada ya chakula haitapelekwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako