• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa madini wa Sudan asema nchi hiyo itapunguza uuzaji wa madini nje

    (GMT+08:00) 2017-07-10 19:11:39

    Waziri wa madini wa Sudan Bw. Hashim Ali Salim amesema, wizara hiyo inapanga kupunguza uuzaji wa madini nje ya nchi.

    Akizungumza na wawekezaji katika sekta ya madini nchini humo mjini Khartoum, waziri huyo amesema moja ya sera muhimu ya serikali ya awamu mpya ni kupunguza uuzaji wa maliasili ya madini nje ya nchi, huku akiongeza kuwa kipaumbele ni kushughulikia madini hayo nchini, na kuwakaribisha wawakezaji wenye nia kushughulikia madini hayo nchini Sudan.

    Mwaka 2011 tangu Sudan Kusini ipatie uhuru, mapato ya Sudan yanayotokana na mafuta yamepungua kwa kiasi kikubwa. Ili kuziba pengo la mapato hayo, serikali ya Sudan imetoa sera na sheria kadhaa kuwashawishi wawekezaji katika sekta ya madini, na kufanya juhudi ya kuinua uzalishaji wa madini ikiwemo dhahabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako