• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OPEC yaunga mkono Makubaliano ya Paris

    (GMT+08:00) 2017-07-10 19:14:15

    Katibu mkuu wa Shirika la Nchi Zinazozalisha Mafuta Duniani OPEC Bw. Mohammed Barkindo amesema, nchi wanachama wa shirika hilo zinaunga mkono msimamo wa kundi la G20 kuhusu Makubaliano ya Paris.

    Bw. Barkindo amesema hayo wakati akihudhuria mkutano wa 22 wa dunia wa mafuta uliofanyika huko Istanbul, Uturuki. Ameongeza kuwa ingawa Marekani imejitoa kutoka makubaliano ya Paris, lakini nchi wanachama wengine 19 zimekubaliana kuwa makubaliano hayo yataendelea. Pia amesema, nchi wanachama wa shirika hilo wamesaini makubaliano hayo.

    Mkutano huo ulikuwa na kaulimbiu ya jinsi ya kukabiliana na changamoto katika sekta ya mafuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako