• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda imepata franc bilioni 136 kupambana na umaskini na kukuza biashara

    (GMT+08:00) 2017-07-10 20:03:46

    Rwanda na Uingereza, kupitia Idara ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID), wametia saini makubaliano ya ushirikiano wa maendeleo yenye thamani ya dola bilioni 136 ili kuharakisha mipango ya maendeleo ya nchi na kukuza ukuaji.

    Franc bilioni 69 zitatumika mwaka huu wa fedha, na franc bilioni 67 ina pangiwa kutumika mwaka ujao wa fedha.

    Mkataba wa miaka miwili unaangalia kusaidia miradi yakupunguza umasikini na kuboresha mapato ya watu, kulingana na Amb Claver Gatete, Waziri wa Fedha na Mipango.

    Aliongezea kuwa msaada huo utasaidia kuimarisha viungo vya biashara vya Rwanda na ushirikiano wake katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na uchumi wa dunia, na pia kusaidia kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya Rwanda na Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako