• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya umoja wa mataifa yathibitisha kuboreka kwa hali ya usalama katika jimbo la Darfur

    (GMT+08:00) 2017-07-11 09:31:24

    Tume ya umoja wa mataifa katika jimbo la Darfur UNAMID imethibitisha kuwa hali ya usalama na hali ya kibinadamu katika jimbo la Darfur nchini Sudan, imeboreshwa, lakini imeonya kuwa hali bado ni tete.

    Mwakilishi maalum wa UNAMID Bw Jeremiah Mamabolo amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa mapambano sasa yamebaki kwenye maficho ya kundi SLA-Abdul Wahid katika eneo la Jebel Marra.

    Hata hivyo bado kuna watu milioni 2.7 wanaoishi kwenye kambi za wakimbizi, makundi yenye silaha bado yako hai, na vurugu za kikabila bado zinaendelea kutokea. Mwakilishi wa UNAMID amesisitiza haja ya kuwa na tahadhari na kuhakikisha hatua zilizochukuliwa zinahakikisha hali ya utulivu kuwa endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako