• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia kuzindua maeneo mawili ya viwanda yaliyojengwa na China

    (GMT+08:00) 2017-07-11 09:31:52

    Taarifa iliyotolewa na waziri wa mipango ya uchumi kwenye ofisi ya waziri mkuu wa Ethiopia Bw Tadese Haile,inasema Ethiopia inatarajiwa kufungua maeneo mawili ya viwanda yaliyojengwa na China, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuifanya nchi hiyo iwe nchi ya viwanda.

    Maeneo hayo ni Dire Dawa kilometa 446 mashariki mwa Addis Ababa, na Adama kilometa 99 mashariki mwa Addis Ababa. Maeneo hayo yamejengwa na kampuni ya uhandisi ya China CCECC kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 190 na 125 mtawalia.

    Lengo la kuwa na maeneo hayo ya viwanda ni kutimiza lengo la Ethiopia kuwa mzalishaji mkubwa wa nguo na sekta ya nguo kuleta pato la dola za kimarekani bilioni 1 kabla ya mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako