• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Iraq atangaza kukombolewa kwa mji wa Mosul

    (GMT+08:00) 2017-07-11 09:44:24

     

    Waziri mkuu wa Iraq Bw Haider al-Abadi ametangaza kuwa utawala wa Kundi la IS mjini Mosul umepinduliwa, na mji wa Mosul sasa umekombolewa.

    Bw al-Abadi amehudhuria na kuhutubia hafla ya kusherehekea ushindi huo, akisema jeshi la Iraq limefanikiwa kuukomboa mji wa Mosul, na kuliondoa kabisa kundi la IS kutoka mjini humo.

    Bw al-Abadi ametoa wito kwa wananchi wote washikamane na kuendelea kupambana na ugaidi ili kuikomboa miji mingine inayodhibitiwa na waasi.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw António Guterres ametoa taarifa akipongeza ukombozi wa Mosul na kuutaja kuwa ni hatua muhimu katika mapambano dhidi ya ugaid. Pia amesema Umoja wa Mataifa unapenda kuisaidia Iraq kuwarejesha wakimbizi makwao, kujenga upya utawala wa kisheria, kuzuia vurugu na kuadhibu kisheria vitendo vya uhalifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako