• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Duru mpya ya mazungumzo ya amani kuhusu suala la Syria yaanza Geneva

    (GMT+08:00) 2017-07-11 09:44:48

    Duru mpya ya mazungumzo ya amani kuhusu suala la Syria yameanza jana mjini Geneva. Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Syria Bw Staffan de Mistura amekutana na ujumbe wa serikali ya Syria.

    Katika mkutano na waandishi wa habari Bw Staffan de Mistura amesema madhumuni ya mazungumzo hayo ni kufikia makubaliano mapya kwa msingi wa makubaliano yaliyofikiwa awali.

    Amesema mapambano yaliyodumu kwa zaidi ya miaka sita nchini Syria ni suala gumu, na umoja wa Mataifa utasaidia kulirahisisha suala hilo katika mazungumzo yafuatayo, ili kuhimiza pande zote kufikia makubaliano.

    Mazungumzo hayo yamefanyika baada ya kuanza kutekelezwa kwa makubaliano ya kusimamisha vita kusini magharibi mwa Syria yaliyosainiwa na Marekani, Russia na Jordan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako