• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia kusajili vyama vya kisiasa kwa ajili ya uchaguzi wa 2021

    (GMT+08:00) 2017-07-11 09:47:11

    Somalia ikishirikiana na wadau mbalimbali ina mpango wa kuboresha mfumo wa vyama vingi vya siasa kupitia kusajili vyama hivyo kabla ya uchaguzi wa mwaka 2021.

    Akiongea kwenye warsha mjini Nairobi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Somalia NIEC, Bibi Halima Ibrahim amesema usajili wa vyama venye sera nzuri na muundo wa kisheria, utafungua njia ya kutambua ubora wa "mtu mmoja, kura moja" wenye lengo la kukuza demokrasia shirikishi nchini humo.

    Amesisitiza kuwa Somalia imedhamiria kupata wataalamu kutoka Afrika na nchi za Kiarabu kwenye masuala ya ujenzi wa taasisi za kisiasa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka mingi.

    Mwezi Septemba mwaka jana serikali ya Somalia ilipitisha sheria ya kuongoza usajili na kanuni za vyama vya siasa, ya "mtu mmoja, kura moja" kabla ya uchaguzi wa 2021.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako