• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kutekeleza sheria ya kupambana na bidhaa zisizo na viwango ili kulinda viwanda vya ndani

    (GMT+08:00) 2017-07-11 09:50:24

    Kenya iko katika mchakato wa kutekeleza sheria ya kupambana na uingizwaji wa bidhaa zisizo na viwango, ili kulinda viwanda vya ndani kutokana na uagizaji wa bidhaa za bei nafuu.

    Akizungumza mjini Nairobi kwenye uzinduzi wa wiki ya biashara, waziri wa viwanda, biashara na vyama vya ushirika Bw Adan Mohammed amesema bunge limetayarisha muswada wa Biashara na linasubiri kusainiwa na Rais kabla ya mwisho wa mwaka.

    Bwana Adan amesema sheria hiyo itakapoanza kutekelezwa, itaweza kulinda soko la ndani na viwanda kutokana na vitendo vibaya vya biashara, vinavyotokana na kuuza bidhaa kwa bei ya chini na ruzuku kutoka nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako