• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini kusaini makubaliano ya eneo la biashara huria ya pande tatu

    (GMT+08:00) 2017-07-11 10:07:11

    Afrika Kusini imetangaza kusaini rasmi makubaliano ya eneo la biashara huria kati ya pande tatu. Wizara ya biashara ya Afrika Kusini imesema, viambatisho vyote vya makubaliano hayo vimepitishwa kwenye mkutano wa mawaziri wa eneo la biashara huria ya pande tatu. Afrika Kusini imekuwa nchi ya 19 iliyosaini makubaliano hayo ambayo yatapunguza ushuru wa biashara na kutoa fursa mpya kwa uuzaji bidhaa nje kwenye soko hilo la pamoja lenye watu milioni 625.

    Habari zinasema Afrika Kusini ikiwa ni nchi mwanachama muhimu ya soko la pamoja la nchi za kusini mwa Afrika COMESA, katika hatua ijayo itasukuma mbele mazungumzo ya ushuru na Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kupunguza ushuru wa biashara kati ya nchi za Kusini na za mashariki mwa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako