• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gor ya Kenya yapata Kocha mpya

    (GMT+08:00) 2017-07-11 10:09:30
    KLABU ya Gor Mahia imepata rasmi Muingereza Dylan Kerr kuwa kocha wake mpya Jumatatu.

    Katika hafla iliofanywa kwa haraka na mabingwa hao mara 15 wa Kenya katika hoteli moja jijini Nairobi, Mwenyekiti wa Gor, Ambrose Rachier, alimsifu Kerr kama kocha aliye na ujuzi mwingi katika kuzinoa klabu za Afrika pamoja na nje ya bara hili.

    Rachier alifichua kuwa Kerr, ambaye aliwahi kuongoza miamba wa Tanzania, Simba SC, amesaini kandarasi ya miaka miwili na uwezekano kuiongeza kutegemea na matokeo atakayopata.

    Kwa upande wake, Kerr alisema hakusita kukubali kuiongoza Gor ilipobisha mlango wake na kuongeza kuwa yuko tayari kuifanyia kazi ili iweze kupata tena umaarufu uliopotea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako