• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 8 wauawa katika shambulizi la guruneti Burundi

    (GMT+08:00) 2017-07-11 10:10:39

    Polisi wa Burundi wamesema, watu wasiojulikana wamefanya shambulizi la guruneti katika mkoa wa Kayanza, kaskazini mwa Burundi jumapili usiku, na kusababisha vifo vya watu 8 na wengine zaidi 50 kujeruhiwa.

    Msemaji wa polisi ya Burundi Bw Pierre Nkurikiye amesema, shambulizi hilo lilitokea saa 12 na nusu jioni katika baa moja. Watu wanne waliuawa papo hapo na wengine 54 wamejeruhiwa, wengi wao wamejeruhiwa vibaya. Majeruhi wanne walifariki dunia jana asubuhi.

    Amesema shambulizi hilo lilimlenga mkuu wa kituo cha kukoboa kahawa cha Kayanza, Claude Nzambimana, ambaye hakujeruhiwa lakini gari lake limeharibiwa.

    Hilo ni moja ya mashambulizi makubwa kuwahi kutokea nchini humo katika miezi kadhaa iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako