• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuhimiza maendeleo yenye mchanganyiko wa kina wa viwanda vya utengenezaji na Mtandao wa Internet

    (GMT+08:00) 2017-07-11 17:56:14

    Mkutano wa Mtandao wa Internet wa mwaka 2017 umefanyika leo hapa Beijing. Waziri wa viwanda na upashanaji wa habari ya China Bw. Miao Wei amesema kwenye mkutano huo kuwa, China itasukuma mbele maendeleo yenye mchanganyiko wa kina wa viwanda na mtandao wa Internet, kuimarisha msukumo wa miundo mbinu ya mtandao wa Internet, kuongeza uwezo wa kulinda usalama wa mtandao wa Internet na upashanaji wa habari, ili kuhimiza njia mpya za viwanda za kufanya uzalishaji wa aina mpya.

    Waziri wa viwanda na upashanaji wa habari Bw. Miao Wei amesema kwenye mkutano huo wa siku tatu wenye kauli mbiu ya "kuunganisha sekta mbalimbali, kuingiza msukumo mpya, na kuungansha viwanda mbalimbali", ingawa bado kuna muda si mrefu tangu kuanzishwa kwa mambo ya mtandao wa Internet nchini China ikilinganishwa na nchi nyingine duniani, lakini baada ya utafiti wa miongo kadhaa, mambo hayo yamepata maendeleo kwa kasi na kuwa viwanda vinavyoongoza nchi nyingine duniani katika pande za miundo mbinu, idadi ya watumiaji na soko. Bw. Miao Wei anasema:

    "China ina mtandao wa Internet unaohusisha eneo kubwa zaidi duniani, na idadi kubwa zaidi ya watumiaji, na soko kubwa zaidi la upashanaji habari ambalo linaongezeka kwa kasi zaidi, na baadhi ya kampuni zimeorodheshwa kati kampuni kubwa zaidi ya mtandao wa Internet duniani, na aina mpya na mifumo mipya ya mtandao wa Internet pia imeonekana kwa wingi, huku usimamizi katika sekta ya mtandao wa Internet ukizidi kuboreshwa."

    Bw. Miao Wei ameeleza kuwa mtandao wa Internet umekuwa sekta yenye uvumbuzi zaidi na kuhusisha sekta nyingi zaidi. Amesema, katika kipindi kijacho, China itazidi kuhimiza maendeleo yenye mchanganyiko wa kina kati ya viwanda na mtandao wa Internet, ili kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo ya aina mpya za viwanda na hali ya viwanda. Bw. Miao Wei anasema:

    "Inapaswa kutekeleza kwa kina uwezo wa akili na kujenga eneo la kielelezo la utengenezaji kwa kutumia uwezo wa akili na mtandao wa Internet; kukamilisha utaratibu wa kiwango kinachounganisha viwanda na upashanaji wa habari, na kuharakisha hatua ya kuhimiza sekta hiyo kufikia katika kiwango cha kimataifa."

    Habari zinasema China itaharakisha ujenzi wa mtandao wa All - optical na WIFI, kuimarisha utafiti na uendelezaji wa teknolojia ya 5G, na kuhimiza uwekaji wa matumizi ya kibiashara ya aina mpya ya mtandao wa Internet na utafiti na uendelezaji wa aina mpya ya muundo, na kutunga mikakati ya maendeleo ya viwanda vya mtandao wa Internet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako