Waziri wa mambo ya nje wa Algeria Bw. Abedel Kader Messahel amesema, wahamiaji haramu wanatishia usalama wa nchi hiyo, na kwamba serikali itachukua hatua za dharura kudhibiti kuingia kwa wahamiaji haramu.
Bw. Messahel amesema hayo jana mjini Algiers alipohutubia mkutano wa kimataifa wa kupambana na ugaidi. Amesema kuwa mtandao wa makundi ya uhalifu ya kimataifa yalikusanya wahamiaji haramu na kuwaingiza nchini Algeria, na nchi hiyo imekua moja ya nchi ambazo wahamiaji haramu kutoka nchi za kusini mwa Sahara wanalenga kuhamia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |