• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wazipongeza Marekani, Russia na Jordan kwa kufikia makubaliano ya kusimamisha vita kusini magharibi mwa Syria

    (GMT+08:00) 2017-07-11 18:29:40
    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amezipongeza Marekani, Russia na Jordan kwa kufikia makubaliano ya kusimamisha vita na kuhimiza uokoaji wa binadamu kusini magharibi mwa Syria.

    Taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake imesema, Bw. Guterres amesema makubaliano hayo ni hatua muhimu katika kusaidia kupunguza mgogoro wa mabavu, kuongeza njia ya uokoaji na kutimiza kusimamisha vita kwa pande zote nchini Syria.

    Taarifa hiyo pia imesema, sasa ni kipindi cha duru mpya ya mazungumzo ya amani ya Geneva kuhusu suala la Syria, na Bw. Guterres amezitaka pande zote zifanye juhudi zaidi kutatua mgogoro wa Syria kwa njia ya siasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako