• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chuo cha China kutoa elimu ya ufundi nchini Rwanda

    (GMT+08:00) 2017-07-11 19:00:11

    Chuo cha ufundi cha Jinhua cha China kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi cha Musanze kimezindua chuo cha kimataifa cha Musanze katika wilaya ya Musanze iliyoko mkoa wa Kaskazini nchini Rwanda, ambacho kitaunganisha mafunzo ya kichina na masomo ya kiufundi, ili kuisadia nchi hiyo kuandaa watu wenye ujuzi na ufundi.

    Chuo hicho kinatarajiwa kuanza kuwaandikisha wanafunzi mwezi Septemba mwaka huu, ambapo wanafunzi watakaochaguliwa watajifunza lugha ya kichina kwa mwaka mmoja, baadaye watakwenda chuo cha ufundi cha Jinhua cha China kujifunza utengenezaji wa mashine, teknolojia ya habari, usimamizi wa hoteli, ujenzi na kilimo.

    Mbali na hayo, chuo hicho pia kimezindua kituo cha maendeleo ya ufundi, ambacho kitasaidia kuwaandaa wafanyakazi wenye ufundi wa huko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako