• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utamaduni wa tiba ya jadi ya China waingia katika shirika la UNESCO

    (GMT+08:00) 2017-07-11 19:01:20

    Siku ya utamaduni wa tiba ya jadi ya China iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Tiba ya Jadi ya China cha Beijing imefanyika katika makao makuu ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO.

    Wataalamu, wasomi na wapenzi wa utamaduni wa China kutoka Ulaya, Asia na Afrika wameshiriki kwenye shughuli hiyo inayolenga kusambaza utamaduni wa tiba ya jadi ya China na kuhimiza dawa za jadi za China kuingia kwenye soko la dunia. Kwenye shughuli hiyo, wataalamu na wasomi kutoka chuo kikuu cha Tiba ya Jadi ya China cha Beijing wamejulisha fursa na changamoto zinazoikabili tiba ya jadi ya China, na kuwafahamisha watu kuhusu mchango wa usingaji na akupancha katika kinga na tiba ya magonjwa na kuboresha afya.

    Mkuu wa chuo kikuu hicho Bw. Xu Anlong amesema, utamaduni wa tiba ya jadi ya China ni sehemu muhimu ya mkakati wa maendeleo wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako