• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Marekani lasema ukombozi wa Mosul haumaanishi kumalizika kwa operesheni ya kupambana na ugaidi

    (GMT+08:00) 2017-07-11 19:02:05

    Wizara ya ulinzi ya Marekani imethibitisha kuwa kituo cha kundi la IS kilichoko Mosul nchini Iraq kimedhibitiwa na kikosi cha usalama cha Iraq, lakini ukombozi wa Mosul haumaanishi kumalizika kwa operesheni ya kupambana na ugaidi.

    Taarifa ya wizara hiyo imesema, wapiganaji wa kundi la IS wanaweza kujificha katika mji mkongwe wa Mosul na mabomu yaliyotegwa kwenye mji mkongwe huo bado yanatakiwa kuondolewa.

    Taarifa hiyo pia imesema, Marekani inazitaka pande mbalimbali za Iraq kushikamana na kupambana na kundi la IS katika sehemu nyingine, ili kuhakikisha mazingira yanayofaa ugaidi hayatokei tena.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako