• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji watano wa kundi la Taliban wauawa mashariki mwa Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-07-11 19:06:38

    Wapiganaji watano wa kundi la Taliban akiwemo kamanda muhimu wa kundi hilo aliyefahamika kwa jina la Azam Gul wameuawa leo katika mapigano na vikosi vya usalana vya Afghanistan katika mkoa wa Laghman ulioko mashariki mwa nchi hiyo.

    Taarifa iliyotolewa na serikali ya mkoa huo imesema, wapiganaji hao walivamia baadhi ya vituo vya ukaguzi vya polisi katika wilaya ya Alishing leo asubuhi, ambapo vikosi vya usalama vilikabiliana nao na kusababisha wapiganaji wengine 6 kujeruhiwa. Pia taarifa hiyo imethibitisha kuwa askari polisi wawili wameuawa na wengine watano kujeruhiwa katika mapigano hayo yaliyodumu kwa saa kadhaa.

    Azam Gul alihusika na kupanga mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama, kutega mabomu kando ya barabara na kulenga maeneo ya serikali. Taarifa hiyo imesema kifo chake kinaweza kuwa pigo kubwa kwa wapiganaji wa Taliban katika mikoa ya Laghman na Nangarhar.

    Kundi la Taliban halijatoa tamko lolote kuhusiana na taarifa hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako