• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yafanya shambulizi la anga dhidi ya kundi la Al Shabaab katika msitu wa Boni

    (GMT+08:00) 2017-07-11 19:16:00

    Jeshi la Kenya limefanya mashambulizi ya anga dhidi ya wapiganaji wa kundi la Al Shabaab wanaoaminika kufanya shughuli zao ndani ya msitu wa Boni ulioko kaunti ya Lamu karibu na mpaka wa Somalia.

    Mratibu wa kanda ya pwani Nelson Marwa amethibitisha kuanza kwa mashambulizi hayo, akisema operesheni hiyo itaendelea licha ya upinzani kutoka kwa baadhi ya Wakenya.

    Eneo la Lamu limeshuhudia mashambulizi kadhaa yaliyosababisha vifo vya watu ndani ya wiki moja iliyopita, tisa kati ya watu hao wakiuawa kwa kukatwa vichwa na magaidi.

    Operesheni hiyo inafanyika siku moja baada ya serikali kuweka amri ya kutotembea usiku katika eneo hilo ikiwa ni moja ya juhudi za kukabiliana na mashambulizi ya kundi la Al Shabaab.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako