• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Wauguzi kuendelea na mgomo

    (GMT+08:00) 2017-07-11 19:18:29

    Chama cha kitaifa cha wauguzi kinasisitiza kwamba hakitasitisha mgomo unaoendelea wa wauguzi hadi serikali itakapotia saini makubaliano nao.

    Katibu mkuu wa chama hicho Maurice Opetu alisema serikali inajikokota katika kushughulikia mzozo huo na akasema chama hicho kinaendelea kutetea maslahi ya wauguzi ili kuhakikisha wanalipwa vyema.

    Wauguzi hao sasa wanatoa wito kwa wizara ya leba iingilie kati na kusuluhisha mzozo huo ili waweze kurejea kazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako