• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda :Uganda yaanzisha kampeini za uwekezaji na uwekaji akiba ya fedha

    (GMT+08:00) 2017-07-11 19:20:10

    Benki ya dfcu ikishirikiana na shirika la Pricewaterhouse coopers wamezindua kampeini ya kitaifa ya kuhimiza uwekezaji na uwekaji akiba.

    Kampeini hii imezinduliwa kwa mashindano ya kushindania fedha na zawadi katika miko yote Uganda.

    Ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika mashariki,Uganda ina kiwango kichache zaidi za watu wanaohifadhi fedha ikiwa ni asilimi 13.48 ya waganda ambao hawasajiliwa na benki.

    Kwa mujibu wa takwimu za shirika la takwimu la Uganda,asilimia 12 ya waganda wana akaunti za benki na pia kuonyesha kwamba waganda huhifadhi chini ya asilimia 5 ya mshahara wao wa kila mwezi.

    Kenya inaongoza kwa uwekaji wa fedha za akiba kwa asilimia 23,Tanzania 13 na Rwanda asilimia 18.

    Benki ya dfcu imeanzisha mipango ya vikundi vya kuweka akiba tangu mwaka 2007 .

    Meneja wa benki hiyo amesema mpango huo utawasaidia wanawake na vijana wanaotafuta fedha za mtaji wa kujiajiri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako