• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la IS lathibitisha kifo cha Abu Bakr al-Baghdadi

    (GMT+08:00) 2017-07-11 21:03:24

    Vyombo vya habari vya Iraq vimesema, kundi la IS limetoa taarifa fupi ikithibitisha kifo cha kiongozi chake Abu Bakr al-Baghdadi na kusema kundi hilo litachagua kiongozi mpya baadaye, lakini taarifa hiyo haikueleza kwa undani kuhusu kifo cha kiongozi huyo.

    Mwezi uliopita, vyombo vya habari vya Russia viliripoti kuwa al-Baghdadi huenda amefariki katika shambulizi lililofanywa na ndege za kivita za jeshi la Russia nchini Syria.

    Lakini habari hiyo haikuthibitishwa na Marekani na Iraq.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako