• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 630 wa Syria warejea makwao mkoani Homs kutoka eneo lililodhibitiwa na waasi

    (GMT+08:00) 2017-07-12 09:36:25

    Shirika la Habari la Syria SANA limeripoti kuwa watu 630 wamerejea makwao mkoani Homs kutoka mji wa kaskazini uliodhibitiwa na waasi.

    Habari zinasema watu hao waliondoka eneo la al-Waer mjini Homs mwezi Mei mwaka jana na kuhamia mji wa Jarablus, kaskazini mwa Syria uliokuwa unadhibitiwa na waasi.

    Mwezi Mei mwaka jana, serikali ya Syria na kundi la waasi walifikia makubaliano ya uhamiaji huo huko al-Waer, eneo la mwisho linalodhibitiwa na waasi mkoani Homs. Makubaliano hayo yameruhusu waasi na familia zao pamoja na wananchi kwenda mji wa Jarablus, kaskazini mwa mkoa wa Aleppo.

    Watu hao 630 wamerejea makwao kutokana na hali ngumu ya Jarablus, ambako walikuwa wanaishi kwenye kambi za waasi wanaoungwa mkono na Uturuki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako