• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Rwanda yakanusha ripoti kuwa wanyarwanda wanaishi kwa hofu

    (GMT+08:00) 2017-07-12 09:36:59

    Serikali ya Rwanda imekanusha ripoti ya Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International inayosema, wanyarwanda wanaishi kwenye mazingira ya hofu wakati nchi hiyo inaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi ujao.

    Ripori hiyo inasema tangu chama tawala cha Rwanda RPF kichukue madaraka miaka 23 iliyopita, wanyarwanda wamekuwa wakikumbana na vikwazo mbalimbali kwenye kujihusisha na mambo ya umma na kukosoa sera ya serikali.

    Waziri wa sheria na mwanasheria mkuu Bw Johnston Busingye amesema ripoti hiyo haina msingi, na lengo lake ni kuvutia ufuatiliaji wa watoa fedha kwa waandishi wa ripoti hiyo. Amesema habari hasi zinazoenezwa kuhusu Rwanda haziwezi kurudisha nyuma maendeleo ya nchi hiyo.

    Wiki iliyopita tume ya uchaguzi ya Rwanda ilitangaza wagombea urais watatu katika uchaguzi wa mkuu wa Rwanda wakiwa ni Rais Paul Kagame wa chama cha RPF, Frank Habineza wa chama cha kijani na Philippe Mpyayimana akiwa mgombea huru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako