• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa Rwanda wakutana kujadili hatua za kuimarisha usalama wakati wa uchaguzi

    (GMT+08:00) 2017-07-12 09:37:21

    Maofisa kutoka wizara ya sheria, tume ya uchaguzi na polisi wa Rwanda, wamekutana mjini Kigali kujadili na kupanga pamoja hatua za kuhakikisha usalama wakati wa uchaguzi mkuu wa Rwanda.

    Waziri wa sheria Bw Johnston Busingye aliyeendesha mkutano wa maofisa hao, amesema katika kipindi cha miaka 23 iliyopita uchaguzi nchini Rwanda umekuwa ukifanyika katika hali nzuri, yenye utulivu na amani, na inatarajiwa kuwa uchaguzi utakaofanyika mwezi Agosti utafanyika katika hali hiyohiyo.

    Pia amevitaka vyombo vya habari visieneze uvumi wenye lengo la kuharibu amani na utulivu wakati wa uchaguzi mkuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako