• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa UNFPA watoa wito wa uwekezaji zaidi katika uzazi wa mpango

    (GMT+08:00) 2017-07-12 09:48:39

    Ofisa mwandamizi wa Shirika la idadi ya watu la umoja wa mataifa (UNFPA) nchini Ghana Bibi Erika Godson, amehimiza kuwepo kwa uwekezaji zaidi katika huduma za uzazi wa mpango.

    Amesema mbali na kuboresha afya na haki, uwekezaji huo pia unaweza kuchochea maendeleo na ni muhimu katika kufanikisha kufikiwa kwa ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu na malengo mengine 17.

    Shirika hilo limesema hayo wakati Burundi inajivunia mafanikio ya matumizi ya uzazi wa mpango, kwa kutekeleza sera iliyopitishwa mwaka 2011, yenye lengo la kupunguza kasi ya ongezeko la uzazi hadi asilimia 2 ifikapo 2025.

    Kenya nayo imeshinda vikwazo vinavyotokana na upungufu wa fedha, na kuepusha imani za jadi na kukaribia kufikia kutimiza uzazi wa mpango.

    Mwakilishi wa UNFPA nchini Kenya Ademola Olaije amesema upatikanaji wa njia bora za uzazi wa mpango wa kisasa umekuwa na manufaa ya kiuchumi, kijamii na kiafya nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako