• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Qatar na Marekani zasaini makubaliano ya kupambana na ufadhili wa ugaidi

    (GMT+08:00) 2017-07-12 09:56:41

    Qatar na Marekani zimesaini makubaliano ya kupambana na ufadhili wa ugaidi mjini Doha. Akizungumza na mwenzake wa Marekani Bw. Rex Tillerson, waziri wa mambo ya nje wa Qatar Bw Mohammed al Thani amesema, Qatar inakaribisha nchi zilizosimamisha uhusiano wa kidiplomasia na Qatar kushiriki kwenye makubaliano hayo yaliyojadiliwa kwa wiki nne.

    Bw. Tillerson amesema Marekani na Qatar zitatoa mchango katika kuchunguza chanzo cha ufadhili kwa ugaidi, kubadilishana taarifa na kuongeza ushirikiano ili kuhakikisha usalama wa kanda hiyo.

    Habari zinasema Bw. Tillerson atakwenda Saudi Arabia kufanya mazungumzo na Saudi Arabia, Misri, Falme za Kiarabu na Bahrain kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi na uhusiano wao na Qatar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako