• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OSCE yajadili njia za kukabiliana na changamoto ya usalama barani Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-07-12 18:34:42

    Mkutano usio rasmi wa mawaziri wa mambo ya nje wa Shirika la Ushirikiano na usalama la Ulaya OSCE umefanyika jana huko Vienna, ambapo mawaziri hao walijadili njia za kukabiliana na mgogoro na changamoto ya usalama wa Ulaya.

    Mwenyekiti wa zamu wa Shirika hilo ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa Austria Bw. Sebastian Kurz amesema, shirika hilo na nchi wanachama wake zinakabiliana na tishio kali la makundi yenye msimamo mkali na yanayotumia nguvu. Amesema jambo la muhimu katika kukabiliana na changamoto ya sasa ni kujenga utaratibu wa mazungumzo ya kina na ushirikiano ili kuratibu vitendo vya pande mbalimbali. Amesema, pande zote zinapaswa kufanya mazungumzo na ushirikiano wa pande mbalimbali, ili kuondoa mikwaruzano iliyoko ndani ya bara la Ulaya kuhusu suala la Ukraine na kuondoa ukosefu wa uaminifu ndani ya shirika hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako