• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wajumbe wa Mkutano wa nishati duniani watoa mwito wa kuhimiza maendeleo ya teknolojia ya nishati

    (GMT+08:00) 2017-07-12 18:38:16

    Wajumbe wa Mkutano wa 22 wa nishati duniani wamesema, kuhimiza maendeleo ya teknolojia na kuzidi kuongeza ufanisi wa nishati ni kipaumbele cha sekta ya nishati katika siku za baadae.

    Ofisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya mafuta ya petrol ya Total ya Ufaransa Bw. Pan Yanlei anayehudhuria mkutano huo amesema, sekta ya nishati inakabiliwa na changamoto tatu kubwa za msukosuko wa uchumi, hali isiyo tulivu ya mambo ya siasa, na mabadiliko ya hali ya hewa, hivyo ni lazima kuongeza fedha ili kukidhi mahitaji ya nishati katika miongo kadhaa ijayo.

    Katibu mtendaji wa Shirika la nishati la kimataifa Bw. Fatih Birol amesema, China, ikiwa nchi inayoongoza nchi nyingine katika sekta ya uendelezaji wa nishati kwa kutumia upepo, jua, nyuklia na kuongeza ufanisi wa nishati, itaonesha kwa mara nyingine tena uwezo wa uongozi kwa kutumia nishati ya barafu mwako ambayo ni nyenzo inayochanganya gesi na maji na kutumiwa kama nishati mbadala ya mafuta ya petrol na gezi katika siku za baadae kutokana na sifa yake ya ufanisi mkubwa wa utoaji wa joto wakati wa kuwaka, kiwango cha chini cha uchafuzi wa mazingira na malimbikizo makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako